• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Aiyabei aweka historia kwenye mbio za Marathon za Frankfurt

    (GMT+08:00) 2019-10-28 08:55:50

    Mwanariadha wa Kenya Valary Aiyabei amekuwa bingwa wa Frankfurt Marathon 2019 kwa kukimbia kwa saa mbili dakika 19 na sekunde 10 na kuvunja rikodi ya saa 2 dakika 20 na sekunde 36 iliyowekwa na Meskerem Assefa na kuwa mwanamke wa kwanza kukimbia chini ya saa 2:20 huko Frankfurt. Kasi ya Aiyabei ni kubwa mara tano katika msimu huu. Amewashinda Waethiopia Megertu Alemu (2:21:00) na Meskerem Assefa (2:22:01) waliochukua nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Assefa alirudi kutetea taji lake lakini alishindwa kuifikia kasi ya Aiyabei. Mwanariadha huo anayefanya mazoezi yake Iten, kaunti ya Elgeyo Marakwet alichomoka kwenye kundi lake la wakimbiaji katika hatua za mwanzo ambako mume wake, Kenneth Kiplagat, naye alikuwa miongoni mwa wakimbiaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako