• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafanikio makubwa yapatikana tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Zambia

    (GMT+08:00) 2019-10-28 09:12:31

    Naibu katibu mkuu wa Shirikisho la Amani kwa Wote Zambia (UPF Zambia) Bw. Lawrence Banda amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika miaka 55 tangu China na Zambia zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Amesema uhusiano huo ulianzishwa kwenye msingi wa kuheshimiana, na utahimiza maendeleo kwenye sekta nyingi za Zambia, hasa ujenzi wa miundombinu. Kwa sasa Zambia imekuwa nchi yenye vifaa vya kisasa vya michezo, barabara, afya na elimu kutokana na ushirikiano huo.

    Ameongeza kuwa China imefanya kazi kubwa katika ujenzi wa miundombinu kwenye nchi za Afrika ikiwemo Zambia, sekta ambayo bado ina changamoto kubwa kwa nchi nyingi za Afrika, na msaada kutoka China utachochea maendeleo ya bara la Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako