• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA: Lewis Hamilton ashinda Mexican GP ila itamlazimu kusubiri kwanza kupata taji la F1

  (GMT+08:00) 2019-10-28 09:19:30

  Lewis Hamilton ameshinda mbio za Mexican Grand Prix huku akifanikiwa kuidhiti kiufundi gari yake katika mbio dhidi ya Ferrari na kuelekea ukingoni kunyakua taji la dunia. Hamilton anaweza kuunyaka ubingwa wa sita kwenye mbio za US Grand Prix Jumapili ijayo kama hakupoteza zaidi ya pointi 22 kwa dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas. Mercedes waliokuwa na wasiwasi wa gari zao kupata ushindi kutokana na mazingira ya Mexico walimshuhudia Hamilton akipambana kiume, katika mbio zilizotumia ufundi mkubwa kati ya madereva wa Mercedes na Ferrari. Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel amekuwa wa pili, mbele ya Bottas na Charles Leclerc.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako