Balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng ametoa zawadi ya maabara ya Tehama kwa Sekondari ya Benon, iliyoko Kaunti ya Trans-Nzoia, kaskazini magharibi mwa Kenya. Maabara hiyo yenye kompyuta 45 inalenga kurahisisha ufundishaji katika shule hiyo. Bw. Wu amesisitiza umuhimu wa kutoa huduma za teknolojia ya mtandao wa Internet katika maeneo ya vijijini ili kuwasaidia wakenya hususan vijana kutafuta fursa za kujiajiri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |