• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Safaricom 'iliwekewa presha' kuteua Mkenya

  (GMT+08:00) 2019-10-28 19:32:56
  KAIMU Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom Michael Joseph ameungana bodi ya kampuni hiyo ili kuteua Mkenya kwa wadhifa huo kutokana na presha kutoka kwa serikali.

  Akihojiwa katika runinga moja nchini, Bw Joseph amesema bodi hiyo ilifikia uamuzi wa kumteua Peter Ndegwa baada ya uchunguzi wa takriban mwaka mmoja, humu nchini na mataifa ya nje.

  Alielezea imani kuwa Bw Ndegwa atatoa uongozi bora kwa Safaricom ikizingatiwa kuwa ana tajriba kubwa aliyopata katika kampuni nyingi za kimataifa zilizoandikisha ufanisi mkubwa.

  Aidha amesema Ni mara ya kwanza Mkenya atakuwa akiongoza kampuni ya mawasiliano ya Safaricom yenye umri wa miaka 19.

  Serikali inamiliki asilimia 35 ya hisa katika Safaricom sawa na Vodacom kutoka Afrika Kusini huku kampuni ya Vodafone kutoka Uingereza ikimiliki asilimia tano ya hisa. Hisa zingine zinamilikiwa na watu binafsi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako