• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yaipongeza Kenya kwa kuendeleza juhudi za kupambana na ufisadi

    (GMT+08:00) 2019-10-29 08:43:59

    Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika cha Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bw. Abebe Selassie amempongeza rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuongoza vita dhidi ya ufisadi, na kusema Kenya iko kwenye njia sahihi.

    Bw. Abebe aliyefanya mazungumzo na rais Kenyatta mjini Nairobi, amesema IMF inaridhika na ukuaji thabiti wa uchumi wa Kenya uliodumisha kiwango cha kati ya asilimia 5.5 hadi asilimia 6, kutokana na mageuzi ya kifedha yanayoendelea nchini humo.

    Rais Kenyatta wa Kenya ameimarisha mapambano dhidi ya ufisadi, tatizo ambalo limeisumbua serikali yake katika muhula wake wa kwanza, ambapo mabilioni ya dola za kimarekani ya fedha za umma ziliibiwa na mafisadi.

    Rais Kenyatta pia ameishukuru IMF kutokana na uungaji mkono wake wa kiufundi kwa Kenya, akisema shirika hilo linachukua nafasi muhimu katika kuhakikisha utulivu wa uchumi wa nchi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako