• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Tanzania kujenga upya madaraja yaliyobomolewa na mvua kubwa

  (GMT+08:00) 2019-10-29 09:04:29

  Mwenyekiti wa baraza la madiwani la Handeni mkoani Tanga Bw. Twaha Mgaya amesema jeshi la Tanzania litajenga upya madaraja manne yaliyobomolewa na mvua kubwa.

  Bw. Mgaya amesema mvua kubwa iliathiri vibaya maeneo ya pwani mkoani Tanga, ikiwa ni pamoja na Handeni, Korogwe na Muheza, ambako barabara, madaraja, nyumba na mashamba vimeharibiwa vibaya. Madaraja hayo yanayohitaji kujengwa upya ni daraja la Nderema linalounganisha Handeni na Kilindi, pamoja na daraja la Kidereko linalounganisha Handeni na Morogoro. Mbali na hayo, daraja la Sindeni kati ya Handeni na Korogwe, daraja la Magamba kati ya Handeni, Coast na Morogoro pia yameharibiwa vibaya.

  Mkuu wa mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigela amesema itachukua wiki moja kujenga upya maradaja hayo, amewataka watu wawe wavumilivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako