Wadau wa mambo ya usalama wa Somalia wameahidi kuwasimamisha waasi wa kundi la al-Shabab kutumia mabomu yanayotengenezwa kienyeji, ili wasije wakawatisha wanachi wa nchi hiyo.
Wadau hao wametoa taarifa ya pamoja baada ya mkutano wa siku mbili mjini Mogadishu, ambayo imesema mabomu ya kienyeji bado ni silaha kuu kwa magaidi inayotumika dhidi ya tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, vikosi vya usalama vya Somalia na raia walioko kwenye njia ya kupokea msaada. Washiriki kwenye mkutano huo wamesema mabomu hayo yanazuia usafiri wa watu na vitu, pamoja na misaada ya kibinadamu.
Naibu mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Simon Mulongo, amesema kuzuia mabomu ya kienyeji ni jambo muhimu kwa AMISOM katika kupambana na ugaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |