• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • GOFU: Tiger Woods ashinda taji la 82nd PGA Tour na kusawazisha rikodi

  (GMT+08:00) 2019-10-29 09:10:12

  Tiger Woods amesema kurudi kwake baada ya majeraha na kushinda michuano ya Mabingwa ya Zozo na kusawazisha rikodi ya US PGA Tour kumemaliza kipindi chake cha changamoto kubwa katika kibarua chake hicho. Woods alimbana kisawasawa Hideki Matsuyama kwenye uwanja wa gofu wa Accordia wa Narashino Country Club na kusawazisha rikodi ya Sam Snead ya 82 na kuwa nafasi ya sita kwenye viwango vya dunia kutoka nafasi ya 10. Lilikuwa shindano lake la kwanza tangu Wood afanyiwe upasuaji wa goti la kushoto mwezi wa nane na kurejea kwenye mashindano Alhamis akiwa na bogeys tatu mfululizo. Baada ya ushindi wake wa Augusta, Woods, ambaye pia alifanyiwa upasuaji mara nne wa mgongo, alikosa nafasi kwenye PGA Championship na Open Championship. Woods amesema sasa anatarajia kurejea nchini na kushindana kwenye Olimpiki ya 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako