• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwezo wa kuhakikisha utoaji wa nishati wa China waongezeka

    (GMT+08:00) 2019-10-29 18:32:09

    Naibu mkurugenzi wa idara ya mpango katika mamlaka ya nishati ya China Bibi Song Wen amesema, katika miezi 9 iliyopita ya mwaka huu uwezo wa kuhakikisha utoaji wa nishati wa China umeongezeka.

    Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Bibi Song amesema, katika miezi 9 iliyopita, uzalishaji wa mafuta ghafi umefikia tani milioni 143, ambao umeongezeka kwa asilimia 1.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na uzalishaji wa gesi asili umefikia mita za ujazo bilioni 127.7. Ameongeza kuwa uwezo wenye sifa bora wa uzalishaji wa makaa ya mawe umefikiwa, huku migodi 40 ya kisasa ya makaa ya mawe imeidhinishwa, na uwezo wa utoaji wa umeme pia umeongezeka zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako