• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano ya kupinga serikali nchini Iraq yaendelea licha ya hatua za usalama kuchukuliwa

    (GMT+08:00) 2019-10-29 18:38:07

    Maandamano ya kupinga serikali yameendelea mapema leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad na mikoa mingine, huku kukiwa na taarifa zinazokinzana kuhusu vifo vya waandamanaji katika mji wa Karbala.

    Mjumbe wa Tume Huru ya Ngazi ya Juu ya Haki za Binadamu nchini Iraq (IHCHR) Ali al-Bayati amesema, taarifa zilizopokelewa kutoka kwa wanaharakati, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kuhusu vurugu zilizotokea Karbala zinadai kuwa watu 18 waliuawa na wengine zaidi ya 800 kujeruhiwa, huku Idara ya Afya ya Karbala ikisema, mtu mmoja aliuawa katika tukio la uhalifu mbali na sehemu yanakofanyika maandamano hayo.

    Shirika la Habari la Iraq (INA) limenukuu ripoti iliyotolewa na Idara hiyo ikisema kuwa watu 112 wamejeruhiwa katika maandamano hayo usiku wa kuamkia leo, na kuthibitisha kuwa hakuna waandamanaji waliopoteza maisha yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako