• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor Mahia hatujakata tamaa, asisitiza Polack

  (GMT+08:00) 2019-10-29 18:47:02

  Kocha wa Gor Mahia Steve Polack ana matumaini makubwa kwamba klabu hiyo itashinda mechi ya ugenini ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF) dhidi ya DC Motema Pembe itakayochezwa Jumapili hii licha ya kutoka sare ya 1-1 wikendi. Mwingereza huyu amewasifia wachezaji wake kwa kung'aa kwenye mchuano huo japo akakiri kwamba walikosa nafasi nzuri za kufunga mabao mengi na kumaliza kazi nyumbani. Katika mechi hiyo ya Jumapili, K'Ogalo walitangulia kufunga kupitia mshambulizi Yikpe Gnamien huku Motema Pembe ikifungiwa bao la pekee na Wiliam Luezi. Licha ya mlinzi Charles Momanyi kupewa kadi nyekundu, golikipa wa K'Ogalo David Mapigano alidaka penalti ya Bongonga Vinny zikiwa zimesalia dakika 10 mechi ikamilike.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako