• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yataka uwekezaji zaidi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2019-10-29 18:54:07

    Mke wa rais wa Kenya Bi Margaret Kenyatta ametoa wito wa kuongeza uwekezaji katika mapendekezo yaliyotolewa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    Akizungumza katika uzinduzi wa Kituo cha Mpango wa Uvumbuzi wa Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi cha Kenya (KCIC) uliofanyika jana mjini Nairobi, Bi. Kenyatta aliwataka wadau wote ikiwemo sekta binafsi kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha kuwa uvumbuzi wa kiteknolojia ambao ni muhimu kwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa una gharama nafuu na unaweza kufikia jamii zilizo hatarini.

    Amesema ingawa uvumbuzi wa kiteknolojia ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuna masuluhisho mengine ya kiteknolojia ambayo ni vigumu kuwafikia walengwa ambao wanaendelea kuathirika na hali mbaya ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako