• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF yapongeza vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya.

  (GMT+08:00) 2019-10-29 18:55:35
  Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) limeipongeza Kenya katika juhudi zake za kupambana na ufisadi, ikielezea matumaini kuwa nchi hii itashinda vita hivyo. Mkurugenzi wa shirika hilo anayesimamia Ustawi wa Afrika Abebe Selassie, pia alisema wameridhika na kiwango cha ukuaji wa kiuchumi nchini ambacho wakati huu ni kati ya asilimia 5.5 na asilimia 6.0.

  Hali hiyo inatokana na mabadiliko ambayo yanatekelezwa na serikali katika sekta ya usimamizi wa kifedha nchini. Akiongea jana alipokutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi, Mkurugenzi huyo alisema kwamba Kenya inaongoza katika nyanja za mageuzi ya kiuchumi na ukuaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Wakati wa mkutano huo, Rais Kenyatta na Bw Abebe walijadili ushirikiano kati ya Kenya na IMF huku kiongozi wa taifa akisema Kenya itaendelea kufanya kazi na shirika hili kwa minajili ya kufanikisha ajenda zake za maendeleo.

  Rais Kenya aliipongeza IMF kwa kuipa Kenya kuendelea kuisadia serikali kutekeleza miradi yenye manufaa kwa Wakenya.

  Wakati wa mkutano huo, Bw Abebe alimjulisha kwa Rais Kenyatta, Tobias Rasmussen ambaye sasa ndiye atakuwa mwakilishi wa IMF nchini Kenya.

  Bw Rasmussen anachukua pahala pa Jan Mikkelsen ambaye kipindi chake cha kuhudumu kilikamilika mnamo Septemba 13, 2019.

  Rais Kenyatta aliwahakikishia maafisa hao wa IMF kwamba milango yake iko wazi kwa majadiliano ambayo yanalenga kunufaisha taifa hili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako