• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waagizaji magurudumu wapewa onyo Tz.

  (GMT+08:00) 2019-10-29 18:55:55
  Wafanyabiashara wa magurudumu visiwani Zanzibar wameombwa kufuata sheria ya kuagiza bidhaa zenye ubora wa juu ili kuepusha ajali na uchafuzi wa mazingira. Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko , Hassan Khamis Hafidh, aliyasema hayo jana katika mjadala wa kutathmini hali ya magurudumu yanayoingizwa nchini. Alisema kwamba kuagiza magurudumu yenye ubora na viwango, yatasaidia kufikia lengo lililokusudiwa la kuwa na biashara endelevu. Aliongeza kwa kusema kwamba mipira isiyokuwa na viwango bora husababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa ajali zinazotokana na magurudumu hayo kupasuka mara kwa mara na hata kusababisha vifo.

  Ili kuafikia haya, wizara ya viwanda, biashara na masoko imejipanga kuthibiti uingizaji wa mipira isiyo na ubora kwa kuwachukulia hatua za kisheria waagizaji. Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango Zanzibar ZBS, Khatib Mwadini Khatib,alisema si vyema kwa wafanyibiashara kufanya udanganyifu wa kuingiza na kuuza bidhaa ghushi kwani zinaweza kuwaathiri vibaya watumiaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako