• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi zaidi ya 170 kushiriki katika Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China

    (GMT+08:00) 2019-10-29 19:11:16

    Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yatafanyika kuanzia tarehe tano hadi 10 mwezi ujao mjini Shanghai, China. Watu kutoka nchi zaidi ya 170 na mashirika mbalimbali ya kimataifa wanatarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo.

    Mkurugenzi wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, ambaye pia ni naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Binnan ameeleza kuwa, kuandaa maonesho hayo ni uamuzi muhimu wa China katika kufungua mlango zaidi kwa nchi za nje, na pia kutahimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya uchumi na kuboresha maisha ya watu nchini China, anasema,

    "Maonesho hayo ambayo ni makubwa zaidi kuliko maonesho ya mwaka jana yatavutia watu wengi zaidi. Mwaka jana maeneo ya maonesho yalikuwa na mita laki 3 za mraba, na mwaka huu yatakuwa na mita laki 3.6 za mraba. Idadi ya nchi, sehemu, mashirika ya kimataifa na wafanyabiashara zote zimezidi kuliko mwaka jana."

    Maonesho hayo yana maeneo ya kuonesha nchi na bidhaa. Eneo la kuonesha nchi lina mita elfu 30 za mraba, na limechukuliwa na nchi 64 ili kujulisha maendeleo yao ya uchumi, mazingira yao ya biashara na bidhaa zao maalumu. Eneo la kuonesha bidhaa lina mita laki 3.3 za mraba, na kwenye eneo hilo, zaidi ya makampuni 3,000 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 150 duniani yataonesha bidhaa zao ikiwemo vifaa, matumizi, vyakula, afya na huduma. Naibu Mkurugenzi wa kamati ya maandalizi ya maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China, ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa biashara wa China Bw. Ren Hongbin anasema,

    "Idadi ya makampuni ya Marekani yatakayoshiriki kwenye maonesho hayo itafikia 192, ambalo ni ongezeko la asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka jana. Yamechukua eneo la maonesho la mita elfu 47.5 za mraba, ambalo ni kubwa zaidi kuliko makampuni ya nchi nyingine. Hali hii inaonesha kuwa maonesho hayo yamevutia sana makampuni ya Marekani."

    Bw. Ren amesema, kufuatia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye maonesho ya mwaka jana, ufanisi wa maonesho hayo katika kuhimiza biashara na uwekezaji utadhihirika zaidi. Anasema,

    "Kwanza, bidhaa nyingi bora zimeingia nchini China, na kukidhi mahitaji ya wateja wa China. Pili, baada ya kufikia makubaliano ya biashara mwaka jana, baadhi ya makampuni yameongeza uagizaji mwaka huu. Tatu, wakati maonesho hayo yanahimiza ushirikiano wa biashara, pia yamehimiza uwekezaji. Nne, Ushirikiano wa biashara umehimiza uboreshaji wa bidhaa zinazotengenezwa nchini China. Tano, maonesho hayo pia yamejenga jukwaa zuri kwa ajili ya kuongeza ushirikiano na mawasiliano ya biashara kati ya sehemu tofauti nchini China".

    Bw. Ren amesema, kutokana na ushiriki na uungaji mkono wa pande mbalimbali, maonesho hayo yatakuwa bora zaidi na kuwa na ufanisi mkubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako