• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika zatakiwa kupambana kwa pamoja na hatari za kiusalama

  (GMT+08:00) 2019-10-30 08:35:45

  Umoja wa Afrika umezitaka nchi za Afrika na mashirika ya umoja huo kuongeza juhudi za kupambana na changamoto za kiusalama zinazoliweka bara hilo kwenye hatari.

  Akiongea kwenye baraza la watu wenye busara, Kamishna wa Amani na usalama wa Umoja wa Afrika Bw. Smail Chergui amesema Afrika imepata mafanikio makubwa kwenye kuzuia migogoro kupitia kutambua dalili zake haraka na matumizi ya diplomasia ya kuizuia, ili kuepusha kuwa migogoro mikubwa.

  Ametaja baadhi ya matishio kuwa ni kuongezeka kwa mapambano kati ya jamii mbalimbali kutokana na mivutano kati ya wakulima na wafugaji, tofauti za kidini na kikabila, kulalamikia matokeo ya uchaguzi na kuongezeka kwa uhalifu wa kuvuka mipaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako