• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN aifurahia kamati ya katiba ya Syria kwa kufanya mkutano wa kwanza

    (GMT+08:00) 2019-10-30 08:40:52

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa akiifurahia kamati ya katiba ya Syria kwa kuandaa mkutano wa kwanza utakaofanyika leo mjini Geneva.

    Bw. Guterres amesema kuanzishwa kwa kamati ya katiba ya Syria "inayomilikiwa na kuongozwa na raia wa Syria" kutaifanya serikali ya Syria na wajumbe wa kundi la upinzani wakutane, na kupiga hatua ya kwanza kwenye mchakato ya kutatua mgogoro wa Syria.

    Ametarajia pande zote zifanye juhudi za pamoja, na kutafuta ufumbuzi unaolingana na matakwa halali ya raia wote wa Syria, chini ya msingi wa kulinda mamlaka, uhuru, umoja na ukamilifu wa ardhi wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako