• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UM latoa wito wa kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2019-10-30 08:49:53

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Jumanne limeridhia azimio Nambari 2493 la kuimarisha Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, kabla ya maadhimisho ya miaka 20 ya ajenda hiyo.

    Baraza la Usalama limezihimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza ajenda hiyo na vipaumbele vyake kupitia kuhakikisha na kuhimiza ushiriki kamili wenye usawa na wenye maana wa wanawake kwenye hatua zote za mchakato wa amani.

    Mwaka 2000 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio 1325 kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, likisisitiza haja ya kushirikisha zaidi wanawake katika juhudi za kujenga usalama na amani, haswa wale walioathiriwa na migogoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako