• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za Afrika Kusini kuonesha bidhaa kwenye maonesho ya pili ya CIIE

  (GMT+08:00) 2019-10-30 08:59:46

  Naibu waziri wa biashara, viwanda na maendeleo ya uchumi wa Afrika Kusini Bibi Nomalungelo Gina, amesema kampuni za nchi hiyo zitaonesha bidhaa kwenye maonesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China CIIE yatakayofanyika huko Shanghai.

  Bibi Gina amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa kampuni za Afrika Kusini kuingia kwenye soko la China, na kuwa kushiriki kwa mara nyingine kwenye maonesho ya CIIE kutaisaidia Afrika Kusini kuongeza uuzaji wa bidhaa zake kwa China. Pia amesema ushiriki wa Afrika Kusini utasaidia kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati yake na China.

  Bibi Gina amesema China inataka kuagiza bidhaa na huduma zenye thamani zaidi ya dola za kimarekani trilioni 10, hali hii imetoa fursa ya kuingia kwenye soko kubwa la China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako