• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanavijiji wa vijiji 1,000 nchini Nigeria waunganishwa na huduma za televisheni ya Satellite

  (GMT+08:00) 2019-10-30 09:00:12

  Mradi wa "Kuunganisha vijiji elfu kumi kwa huduma za televisheni ya Satellite" nchini Nigeria umetangazwa kukamilika. Wanavijiji wa vijiji elfu moja nchini humo sasa wanaweza kuangalia televisheni ya Satellite.

  Mradi huo ni moja ya hatua za ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya jamii na utamaduni ambazo zilitolewa kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2015. Na lengo lake ni kuvifanya vijiji elfu kumi barani Afrika viweze kupokea matangazo ya televisheni kwa njia ya ya Satellite.

  Mwenyekiti wa kamati ya upashanaji wa habari ya bunge la Nigeria ameishukuru serikali ya China, na kusema mradi huo umewanufaisha raia wa kawaida, na familia nyingi maskini zinaweza kuangalia televisheni kwa njia ya Satellite, na huu ni ushahidi mwingine wa urafiki kati ya Nigeria na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako