• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: IAAF yapanga tarehe ya kusikiliza kesi ya bosi wa zamani wa IAAF Lamine Diack, na mtoto wake

    (GMT+08:00) 2019-10-30 09:02:59

    Mahakama ya Paris Jumatatu imetangaza kuwa inapanga kuanza kusikiliza kesi ya bosi wa zamani wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), Lamine Diack, na mtoto wake Papa Massata Diack kwa kula rushwa kuanzia Januari 13. Lamine Diack, aliyekuwa mkuu wa IAAF kati ya mwaka 1999 na 2015, anashtakiwa kwa kutoa na kupokea rushwa, kuondoa uaminifu na kupanga utakatishaji wa pesa. Papa Massata Diack, aliyekuwa akishughulikia haki muhimu za soko za IAAF, yeye anashutumiwa kuwa mhusika mkuu kwenye mtandao wa ufisadi na kushtakiwa kwa utakatishaji pesa, kutoa rushwa na kusaidia kupokea rushwa. Wawili hao wanatuhumiwa kwa kuwa kiini cha mtandao wa rushwa. Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya mwendesha mashataka wa fedha nchini Ufaransa mwaka 2018 ni pamoja na madai kwamba Lamine Diack amechukua pesa kutoka Russia kwa ajili ya kampeni za kisiasa za Senegal, na badala yake IAAF kusaidia kuficha makosa ya Russia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako