• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutekeleza hatua 20 za kuvutia uwekezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2019-10-30 16:29:10

    Baraza la Serikali la China hivi karibuni limepitisha "pendekezo la namna ya kutumia vizuri uwekezaji wa nje". Kwa mujibu wa pendekezo hilo, China itatekeleza hatua 20 za kufungua mlango zaidi, kuongeza nguvu ya kuhamasisha uwekezaji wa nje, kukuza mageuzi ya kurahisisha uwekezaji, na kuimarisha ulinzi wa maslahi halali ya wawekezaji wa nje.

    Tangu mwanzo wa mwaka huu, kwa nyakati tofauti, China imetekeleza hatua mbalimbali za kuhamasisha uwekezaji kutoka nchi za nje, ikiwemo kupunguza sekta zinazopigwa marufuku kuwekezwa na wawekezaji wa nje, na kujenga maeneo mapya ya majaribio ya biashara huria. Hatua hizo zimefanya kazi chanya katika kuvutia uwekezaji wa nje na kuongeza sifa ya uwekezaji huo. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shouwen amesema, China itaendelea kuinua kiwango cha kuhimiza na kulinda uwekezaji wa nje. Anasema,

    "Katika upande wa kufungua mlango zaidi, hatua zitakazotekelezwa na China ni pamoja na kuendelea kupunguza orodha ya sekta zinazopigwa marufuku kuwekezwa na wawekezaji wa nje, kuondoa vikwazo vyote visivyo ndani ya orodha hiyo, kuharakisha mchakato wa kufungua sekta ya fedha, kuboresha sera kuhusu uwekezaji wa nje katika sekta ya magari, na kujitahidi kuanzisha mazingira yenye usawa."

    Kufuatia pendekezo hilo, China inazingatia kuzipa kampuni zenye uwekezaji wa nje haki sawa na kampuni za China, kujitahidi kuanzisha mazingira wazi na ya kuaminika kwa uwekezaji wa nje, na kulenga kudumisha ukubwa wa uwekezaji huo na kuboresha muundo wake. Pia kutilia maanani ufuatiliaji wa kampuni zenye uwekezaji wa nje, kuagiza serikali za mitaa kukuza mageuzi, na kuimarisha zaidi juhudi za kuhimiza na kulinda uwekezaji wa nje.

    China pia imeanza kutekeleza sheria mpya ya uwekezaji wa nje, ili kulinda maslahi halali ya wawekezaji kutoka nchi za nje. Mkurugenzi wa ofisi ya ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu iliyo chini ya idara kuu ya hakimiliki za kiubunifu ya China Bw. Zhang Zhicheng anasema,

    "Katika upande wa sheria, China imehimiza kwa hatua madhubuti ujenzi wa mfumo wa kulipa fidia kutokana na vitendo vya wizi wa hakimiliki za kiubunifu. Hivi sasa muswada wa kurekebisha sheria ya haki za hataza umejadiliwa kwa mara ya kwanza na Kamati ya Kudumu ya Bunge la umma la China."

    Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia inaonesha kuwa, nafasi ya China duniani katika ubora wa mazingira ya kibiashara imepanda kutoka 46 hadi 31.

    Katika miezi tisa iliyopita, China imetumia uwekezaji wa nje wa dola bilioni 100.8 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 2.9 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Bw. Wang anaona kuwa, kutokana na hali ya uchumi wa dunia, matokeo haya ni mazuri, akisema,

    "Soko kubwa na China linavutia sana uwekezaji wa nje. Licha ya hayo, China ina sheria na sera tulivu, wazi na za kuaminika, miundombinu bora na uwezo mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumi, nguvu kazi, na pia inafanya juhudi kubwa ili kulinda hakimiliki za kiubunifu."

    Bw. Wang ameeleza matarajio mazuri kuhusu hali ya kuingiwa kwa uwekezaji wa nje nchini China katika mwaka huu na mwaka ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako