• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wasema uhusiano na China ni muhimu kwa maendeleo ya Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2019-10-30 18:51:16

  Wataalam wanaohudhuria kongamano la kwanza la washauri bingwa wa China na Sudan Kusini lililofanyika mjini Juba, wamesema, mawasiliano yanayoongezeka kati ya Sudan Kusini na China ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya siasa, uchumi na miundombinu ya nchi hiyo.

  Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti kuhusu Afrika ya Chuo Kikuu cha Zhejiang, China, Bw. Liu Hongwu amesema, Sudan Kusini inaweza kujifunza mengi kutoka China katika mapambano dhidi ya umaskini, maendeleo ya uchumi na kuvutia uwekezaji kutoka nje. Amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika hasa katika mafunzo na ujenzi wa miundombinu ni muhimu na unaweza kulifanya bara la Afrika, hususan Sudan Kusini, kujiendeleza kwa kasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako