• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2019-10-30 18:56:58

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limefanya mjadala kuhusu wanawake, amani na usalama, na kupitisha azimio No. 2493 linalotaka kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye michakato mbalimbali ya amani duniani, kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya wanawake, amani na usalama iliyoanzishwa mwaka 2000.

    Azimio hilo linatoa wito wa kutoa urahisi kwa wanawake kushiriki kwenye mazungumzo ya amani, pamoja na kuungwa mkono wakiwa wawakilishi wa mazungumzo na mifumo ya utekelezaji na usimamizi wa makubaliano. Pia limeihimiza kamati ya ujenzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono mashirika husika yanayoongozwa na wanawake kushiriki kwenye kazi ya ukarabati baada ya vita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako