• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka baadhi ya nchi za magharibi kutojifanya walinzi wa haki za binadamu

    (GMT+08:00) 2019-10-30 18:57:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China inazitaka baadhi ya nchi za magharibi kuacha kujifanya walinzi wa haki za binadamu, kuacha kutumia vigezo viwili, na kuingiza mambo ya kisiasa kwenye suala la haki za binadamu, pia kuacha kuingilia kati mambo ya nchi nyingine kwa kisingizio cha haki za binadamu.

    Bw. Geng Shuang amesema, nia ya baadhi ya nchi za magharibi kuipinga China kuhusu suala la haki za binadamu imeshindwa. Amesema hatua mbalimbali za kukinga na kupambana na ugaidi zilizochukuliwa katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur zimebadilisha hali ya usalama ya mkoa huo. Katika miaka mitatu iliyopita, hakuna tukio la kigaidi lililotokea katika eneo hilo, jamii imekuwa tulivu, watu wa makabila mbalimbali wanashikamana, na wanaishi maisha mazuri. Hatua hizo zimehakikisha haki ya kimsingi ya binadamu ya watu wa makabila mbalimbali, na kulinda usalama na utulivu wa eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako