• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na makamu wa rais wa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-10-30 19:01:17

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na makamu wa rais wa Afrika Kusini David Mabuza ambaye yuko ziarani nchini China na kuhudhuria mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati ya pande mbili za China na Afrika Kusini.

    Bw. Li Keqiang amesema, China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini kuongeza kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano na maingiliano ya watu, kusukuma mbele uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na kati ya China na Afrika kupata maendeleo mapya.

    Bw. Mabuza amesema kwa sasa uhusiano kati ya Afrika Kusini na China umedumisha maendeleo ya pande zote, na kuishukuru China kwa kuiunga mkono Afrika Kusini na nchi za Afrika. Amesema Afrika Kusini inapenda kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China, kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kuinua kwenye kiwango kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako