• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bodi ya NHIF ilitumia Sh38 milioni kwa mikutano – Mhasibu

  (GMT+08:00) 2019-10-30 19:39:46
  IMEBAINIKA kwamba Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) ilitumia Sh38 milioni za walipa ushuru kuandaa mikutano ya bodi, warsha na makongamano mwaka 2018.

  Ripoti ya aliyekuwa mkaguzi wa hesabu za serikali Edward Ouko katika mwaka wa kifedha uliokamilika Juni 2018 ilibainisha kwamba, NHIF ilitumia pesa hizo lakini ikakosa kuonyesha stakabadhi za kuthibitisha matumizi hayo.

  Kulingana na stakabadhi zilizopelekwa mbele ya kamati ya uwekezaji katika Bunge la Kitaifa, kati ya fedha hizo, Sh13,115,573 zilitumika kuandaa warsha na makongamano.

  Ingawa usimamizi umefafanua kwamba pesa hizo zilitumika kugharimia mikutano ya bodi, hakukuwa na ushahidi kuthibitisha matumizi hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako