• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaitaka Sudan Kusini itekeleze ahadi kuhusu ubora wa elimu kwa wakimbizi wa ndani

    (GMT+08:00) 2019-10-31 08:21:02

    Jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imeitaka Sudan Kusini kuharakisha kuandaa mpango wa kitaifa wa mwitikio wa elimu, ikiwa ni njia muhimu ya kuhimiza utekelezaji wa maamuzi ya kikanda kuhusu kutoa elimu kwa wakimbizi, watu waliorudi nyumbani na jamii zinazowapokea.

    Taarifa iliyotolewa jana na IGAD inasema mpango huo utakuwa muhimu katika kutekeleza azimio la Djibouti na mwito wa Addis Ababa kuhusu watu hao.

    Mwezi juni mwaka jana nchi wanachama wa IGAD zinazopokea mamilioni ya wakimbizi kutoka kwenye kanda hiyo na nje ya kanda hiyo, zilitaka kuwe na juhudi za makusudi kuwapatia elimu bora wakimbizi wanaoendelea kuongezeka kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako