• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wasema matumizi ya satellite kuhimiza ongezeko la uchumi wa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-10-31 08:21:22

  Kamati ya Umoja wa Afrika imesema mawasiliano kwa njia ya Satellite yana uwezo wa kuhimiza ongezeko la uchumi kwa nchi za Afrika.

  Mkurugenzi wa idara ya raslimali watu, sayansi na teknolojia wa Umoja wa Afrika Bw. Mahama Ouedraogo amesema kuingiza matumizi ya teknolojia ya satellite kutahimiza ongezeko la uchumi na la utekelezaji wa ajenda ya mageuzi.

  Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa mwaka wa masomo ya sera za teknolojia barani Afrika, Bw. Ouedraogo amesema ni bahati mbaya kuwa ushiriki wa Afrika kwenye matumizi ya teknolojia hiyo ni dhaifu sana, wakati teknolojia hiyo inatoa fursa nyingi za maendeleo.

  Amesema kati ya mwaka 1998 na mwaka huu, nchi za Afrika zimerusha satellite 35 tu nyingi zikitumika kwenye maeneo ya ufuatiliaji wa dunia, mawasiliano, kuonesha teknolojia, utafiti wa kisayansi, miradi ya elimu na rada za kijeshi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako