• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Huawei ya China iko tayari kuhimiza mageuzi ya kidijitali katika nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2019-10-31 08:59:17

    Ofisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya Tehama ya China Huawei Bw. Ren Zhengfei, amesema kampuni yake iko tayari kusukuma mbele mageuzi ya kidijitali katika nchi za Afrika, ili kuzisaidia kutimiza maendeleo endelevu ya kiuchumi.

    Akihojiwa na gazeti la Ahram la Misri, Bw. Ren Zhengfei amesema nchi za Afrika zinapaswa kuichukulia teknolojia ya Tehama kuwa mkakati wa kitaifa unaosubiri uratibu wa mipango na matumizi ya mifumo, na kuwekeza zaidi katika miundombinu haswa mkonga wa mawasiliano aina ya optic fiber.

    Bw. Ren ameipongeza Misri kutokana na mageuzi ya kidijitali yanayoendelea nchini humo, akisema mageuzi hayo katika sekta za uchumi na viwanda yana umuhimu mkubwa kwa Misri ambayo sekta ya Tehama itachukua nafasi muhimu katika kuziwezesha sekta nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako