• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Afrika asema China inachangia juhudi za Afrika katika kupambana na Ukimwi

    (GMT+08:00) 2019-10-31 08:59:41

    Ofisa mmoja wa Umoja wa Afrika amesema China imetoa mchango wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja kwenye juhudi za Afrika katika mapambano dhidi ya Ukimwi, kifua kikuu na malaria.

    Kaimu mkurugenzi wa Kitengo cha kupambana na UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria katika Umoja wa Afrika Bw. Benjamin Djoudalbaye amesema mchango wa China kwa mfuko wa kimataifa wa kupambana na magonjwa hayo, ni sehemu ya uungaji mkono usio wa moja kwa moja katika vita dhidi ya Ukimwi barani Afrika.

    Takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinasema Ukimwi unaendelea kuwa suala kuu la afya ya umma duniani. Mwaka jana watu laki 7.7 kote duniani walifariki kutokana na ugonjwa huo. Afrika ikiwa ni bara linaloathiriwa vibaya zaidi na ugonjwa huo, linachangia theluthi mbili za maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako