• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe maalumu wa UN ahimiza mazungumzo kati ya waandamanaji na serikali nchini Iraq

  (GMT+08:00) 2019-10-31 09:15:06

  Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jeanine Hennis-Plasschaert amefanya ziara katika Uwanja wa Tahrir mjini Baghdad, kuhimiza mazungumzo kati ya waandamanaji na serikali nchini humo.

  Taarifa iliyotolewa na tume ya Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI), imesema Hennis-Plasschaert amebadilishana maoni na kujadili njia zinazowezekana kushughulikia madai halali ya waandamanaji wa amani. Ametoa mwito wa kufanya mazungumzo ya kitaifa ili kutafuta njia ya utatuzi, kuvunja mzunguko mbaya wa vurugu, na kuwa na mshikamano dhidi ya hatari ya mgawanyiko na kutoshughulikia changamoto.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako