• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya katiba ya Syria yazinduliwa rasmi huko Geneva

    (GMT+08:00) 2019-10-31 09:15:39

    Tume ya katiba ya Syria iliyoundwa na serikali, wapinzani, na wajumbe wa kiraia nchini humo imezinduliwa rasmi huko Geneva, na kuanza kazi kuhusu mageuzi ya katiba ya nchi hiyo.

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Geir Pedersen siku hiyo kwenye sherehe ya kuzinduliwa kwa tume hiyo amesema, kuzinduliwa kwa tume hiyo kumewafanya wajumbe wa serikali na wapinzani wakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, ambalo ni tukio la kihistoria, na pia linaonesha kuwa msukosuko wa Syria uliodumu kwa karibu miaka 9 umepiga hatua kubwa kuelekea utatuzi wa kisiasa.

    Vilevile amesisitiza kuwa katiba inayowakilisha na kushirikisha pande mbalimbali, inaweza kuponya majeraha yanayosababishwa na migogoro na kuweka msingi kwa suluhu ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako