• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika waimarisha ushirikiano wa juhudi za mabadiliko ya tabianchi

  (GMT+08:00) 2019-10-31 09:47:53

  Mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU) Bibi Fatima Kyari Mohammed amesema Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa wanatakiwa kuongeza juhudi za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

  Bibi Mohamed amesisitiza mahitaji ya kuongeza ushirikiano kwenye mambo ya usalama wa tabianchi kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, haswa katika maeneo ya Sahel, Pembe ya Afrika na maeneo mengine yaliyoathiriwa.

  Amesema athari za mabadiliko ya tabianchi zinazidisha mivutano iliyopo katika maeneo haya, kama inavyoonekana katika kuongezeka kwa mvutano baina ya jamii na mapigano katika sehemu mbalimbali za Afrika. Pia amesema ingawa Umoja wa Afrika umefanya juhudi za kukabiliana na hali hiyo kwa wakati, juhudi za pamoja zinapaswa kuzingatiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako