• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yahimiza waendesha mashtaka wa Afrika Mashariki kushirikiana ili kupambana na uhalifu

  (GMT+08:00) 2019-10-31 09:48:15

  Kenya imetaka waendesha mashtaka wa umma kutoka nchi za Afrika Mashariki kushirikiana ili kupambana na uhalifu wa kupangwa ulioenea katika kanda hiyo.

  Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw. Fred Matiang'i amesema waendesha mashtaka wanatakiwa kutafuta njia za kuongeza ushirikiano kwenye kuendeleza ujuzi na ujenzi wa uwezo, ili kuwafanya waendesha mashtaka wa eneo hilo wawe sehemu ya vikundi vya uchunguzi vya pamoja.

  Bw. Matiang'i amesema hayo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Waendesha Mashtaka wa Afrika Mashariki uliofanyika mjini Mombasa, na kuongeza kuwa changamoto nyingi za kiusalama zinavuka mipaka, na ushirikiano unatakiwa kuwepo katika kuboresha uwezo wa waendesha mashtaka wa kikanda katika kukabiliana na uhalifu uliopo na unaoibuka wa makundi ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako