• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yazindua rasmi matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G

  (GMT+08:00) 2019-10-31 18:22:14

  Wizara ya maendeleo ya viwanda na teknolojia ya habari ya China na Kampuni tatu za upashanaji habari za China leo kwenye maonesho ya kimataifa ya teknolojia za upashanaji habari zimezindua rasmi matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G, ikimaanisha kuwa zama ya 5G imeanza nchini China.

  "Tuanze kwa pamoja mchakato mpya wa matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G."

  Katika siku ya kwanza ya maonesho ya kimataifa ya teknolojia ya upashanaji habari ya China ya mwaka huu, naibu waziri wa maendeleo ya viwanda na teknolojia nchini China Bw. Chen Zhaoxiong akiwa pamoja na wakuu wa kampuni tatu za upashanaji habari za China wamezindua rasmi matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G.

  Bw. Chen anaona kuwa, hivi sasa uchumi wa China umeingia kwenye kipindi cha maendeleo yenye sifa ya juu badala ya kipindi cha maendeleo ya kasi, na kinahitaji teknolojia yenye ufanisi mkubwa zaidi ya kisasa ya upashanaji habari. Amesema kuwa China inaharakisha mchakato wa matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G, ambayo yanapatikana katika miji ya Beijing, Shanghai, Guangzhou, Hangzhou na mingineyo, na inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, vituo vya 5G nchini China vitazidi laki 1.3. Anasema,

  "China inaharakisha kupanga mtandao wa 5G, na kuhimiza kuunganisha teknolojia hiyo mpya na sekta za uchumi, haswa katika viwanda, mawasiliano ya barabara, nishati na kilimo, ili kuongeza injini ya maendeleo ya uchumi."

  Aidha, Bw. Chen amesema, China pia itahimiza uvumbuzi na matumizi ya 5G katika elimu, afya, huduma za serikali na maisha mijini, ili kuboresha njia ya utoaji wa huduma za kijamii.

  Mkuu wa bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Habari Kupitia Simu za Mkononi ya China Bw. Yang Jie amesema, teknolojia ya 5G itakuwa chanzo cha upashanaji wa habari, injini ya uboreshaji wa sekta za uchumi, na msingi wa ujenzi wa jamii ya kidata. Anasema,

  "Mwaka huu kampuni yetu itaunga mtandao wa 5G katika zaidi ya miji 50, na kutoa huduma za kibiashara. Hadi mwaka kesho, tutaanzisha mtandao wa 5G katika miji yote nchini China."

  Naye mkuu wa bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Muungano ya Upashanaji Habari Mtandaoni ya China Bw. Wang Xiaochu amesema, kampuni yake itashirikiana na kampuni za uzalishaji wa simu ya mkononi kutoa simu za aina mbalimbali za 5G, ili kuhimiza matumiza ya teknolojia hiyo.

  Hadi sasa kampuni tatu kuu za upashanaji habari nchini China zimetoa toleo la 5G, ambayo bei chini zaidi ni dola zaidi ya kumi tu. Aidha, kampuni hizo pia zimetangaza miji 50 nchini China ambayo matumizi ya kibiashara ya 5G yataanza kutumika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako