• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Sudan lamaliza luteka ya kijeshi kaskazini mwa Khartoum

  (GMT+08:00) 2019-10-31 18:44:39

  Jeshi la ulinzi la Sudan limemaliza luteka ya kijeshi iliyofanyika kwenye eneo la Shakhout, kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

  Mwenyekiti wa Baraza la Pamoja la Utawala nchini Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Mnadhimu wa Majeshi Luteni Jenerali Mohamed Osman Al-Hussein walihudhuria hafla ya kumalizika kwa zoezi hilo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa mafunzo kwa jeshi la ardhini la nchi hiyo.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Luteni Jenerali al-Burhan amesema, mafunzo hayo yanayoongeza umakini wa kupambana kwa askari na pia kuwajengea kuwaamini makamanda wao.

  Askari kutoka jeshi la ardhini na la anga nchini Sudan walishiriki katika zoezi hilo la kijeshi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako