• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa China atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya amani na utulivu wa Burundi

  (GMT+08:00) 2019-10-31 18:46:40

  Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao jana amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono juhudi za amani, utulivu na maendeleo ya Burundi.

  Amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa zinapaswa kufanya kazi ya kiujenzi kuisaidia Burundi kutimiza amani na utulivu wa kudumu. Ameongeza kuwa, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu haki ya uongozi wa serikali ya Burundi na wananchi wake katika suala la uchaguzi, na kuongeza msaada wa kibinadamu, kijamii na kiuchumi.

  Balozi Wu pia amesema, China siku zote inaunga mkono mchakato wa kisiasa wa Burundi na ukarabati wa nchi hiyo, na kutoa msaada kwa Burundi katika sekta za kilimo, elimu na ujenzi wa miundombinu. China inapenda kuendelea kutoa mchango kwa ajili ya Burundi kutimiza amani, utulivu na maendeleo endelevu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako