• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Falme za Kiarabu yatangaza kuondoa askari mkoani Aden, Yemen

  (GMT+08:00) 2019-10-31 18:48:41

  Kikosi cha jeshi la Falme za Kiarabu kimetangaza kuwa, askari wake waliopelekwa mkoani Aden, nchini Yemen, wamerudi nchini mwao baada ya kumaliza kazi zao.

  Taarifa iliyotolewa na kikosi hicho imesema, askari hao wametoa mafunzo kwa kikosi cha Yemen na kukiongezea uwezo wa kulinda usalama na utulivu, na kuongeza kuwa, hivi sasa, kazi ya kulinda usalama mkoani humo imerudishwa kwa vikosi vya Yemen na Saudi Arabia.

  Taarifa hiyo pia imesema, Falme za Kiarabu itaendelea kushirikiana na wenzi wake wa kikanda kuunga mkono watu wa Yemen kupambana na ugaidi kusini mwa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako