• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yasaini mpango wa kumaliza uandikishaji na matumizi ya askari watoto

    (GMT+08:00) 2019-10-31 18:54:23

    Somalia imesaini mpango unaoainisha hatua za kivitendo za kuzuia ukiukaji wa haki za watoto, kuwaachia huru watoto wanaohusishwa na makundi yenye silaha, na kuwarejesha tena katika jamii.

    Makubaliano hayo yaliyoshuhudiwa na mjumbe maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mapigano ya Kutumia Silaha, Bi. Virginia Gamba, yameonyesha nia ya Somalia ya kumaliza uandikishaji na matumizi ya askari watoto.

    Hatua hii imekuja wakati wasiwasi mkubwa ukiongezeka nchini Somalia kutokana na uandikishaji na matumizi ya askari watoto kama wapiganaji katika mapambano ya silaha na makundi ya kigaidi kama Al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako