• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati ya pande mbili za China na Afrika Kusini wafanyika

    (GMT+08:00) 2019-10-31 19:16:46

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na makamu rais wa Afrika Kusini David Mabuza, na wameendesha kwa pamoja mkutano wa 7 wa wajumbe wote wa kamati ya pande mbili za China na Afrika Kusini.

    Bw. Wang amesema, katika kipindi kijacho, pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha kuaminiana ya kisiasa, kuunga mkono maslahi makuu na mambo yanayofuatiliwa na upande mwingine, na kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimkakati. Pia amesema pande hizo zinapaswa kunufaishana na fursa ya maendeleo, kuanzisha mambo mapya ya ushirikiano, kuimarisha maingiliano ya watu, kuendelea kuhimiza ushirikiano katika elimu ya juu, mafunzo kwa watu, afya na matibabu, utamaduni na utalii. Zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika mifumo ya Umoja wa Mataifa, kundi la G20 na BRICS, kulinda mfumo wa pande nyingi, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kujenga mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya nchi kubwa zinazoendelea.

    Bw. Mabuza amesema Afrika Kusini inapenda kushirikiana na China kufanya kazi ya uongozi ya kamati hiyo katika mambo mbalimbali ya nchi hizo mbili, kuinua kiwango cha ushirikiano kwa pande zote na kuhimiza uhusiano kati ya Afrika Kusini na China kuinuka kwenye kiwango kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako