Ofisa Biashara wa mkoa wa Mbeya,Stanley Kibakaya,alisema hayo wakati wa kikao cha kutathmini mafunzo kwa vijana kilichoitishwa na asasi ya kiraia ya "Saidia Wahitaji Shop" inayotoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kwa kushirikiana na The Foundation for Civil Society.
Alisema lengo la mafunzo ni kuhakikisha vijana hao wananufaika na rasilimali mbalimbali ndani ya maeneo yao na nchini humo kwa ujumla na kuwaepushia tabia ya kukaa vijiweni wakisubiri kuajiriwa.
Kibakaya alisema vijana hao wakizingatia elimu hiyo wanaweza kujiongezea kipato kwa kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitakuwa na tija kwao na kwa serikali kwa madai kuwa zitasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuiongezea serikali kiwango cha ukusanyaji mapato.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |