• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Zambia zapeana salamu za kupongeza miaka 55 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi

  (GMT+08:00) 2019-10-31 20:06:27

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Zambia Joseph Malanji wamepeana salamu za pongezi kuadhimisha miaka 55 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

  Kwenye salamu zake, Bw. Wang amesema, tangu nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibalozi, uhusiano kati yao umedumisha mwelekeo wa maendeleo mazuri, zimezidi kuaminiana kisiasa, ushirikiano umepata matokeo makubwa, na uratibu katika mambo ya kimataifa na ya kikanda umekuwa wa karibu. Amesema, anapenda kushirikiana na Bw. Malanji kuhimiza uhusiano na ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Zambia kuingia kiwango kipya.

  Naye Bw. Malanji amesema, kwa muda mrefu Zambia na China zimeaminiana na kuheshimiana. Zambia inapenda kushirikiana na China kuhimiza utekelezaji wa mapema wa matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako