• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wahimiza sera madhubuti za uhamiaji wa nguvukazi ili kulinda wafanyakazi wahamiaji wa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-01 08:35:17

  Wataalamu na watunga sera wa Afrika wametoa wito wa juhudi za kulinda wafanyakazi wahamiaji wa Afrika wanaoongezeka, haswa wale walioko katika Mashariki ya Kati.

  Wataalamu na watunga sera hao kutoka nchi zenye watu wengi wanaotoka kwenda kufanya kazi katika Mashariki ya Kati na Nchi za Ghuba GCC, wametoa wito huo wa dharura jana Alhamisi kwenye mkutano unaoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

  Mkutano huo ulioandaliwa na Programu ya Usimamizi wa Pamoja wa Uhamiaji wa Nguvukazi kwa ajili ya Maendeleo ya Kikanda na Mafungamano ya Afrika, unatarajia kuhimiza mchakato unaoshirikisha pande mbalimbali kuelekea kuimarisha ulinzi wa wafanyakazi wengi kutoka Afrika katika kanda ya Mashariki ya Kati.

  Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Afrika, Misri, Ethiopia, Kenya, Sudan, Afrika Kusini na Uganda ni nchi zenye watu wengi zaidi wanaofanya kazi Mashariki ya Kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako