• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la wawakilishi la Marekani lapitisha uamuzi wa mchakato wa kumshitaki Rais Trump

  (GMT+08:00) 2019-11-01 08:41:22

  Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani limepitisha azimio lenye lengo la kuhalalisha mchakato wa kumshitaki Rais Donald Trump kwenye baraza hilo. Azimio hilo limepitishwa kwa kura 232 dhidi ya kura 196, hakuna mwakilishi hata mmoja wa chama cha Republican aliyeunga mkono azimio hilo.

  Hii ni mara ya kwanza kwa baraza hilo kupiga kura hiyo tangu spika wake Bibi Nancy Pelosi atoe pendekezo hilo mwezi Septemba. Hatua hiyo inafuatia mtu mmoja kutoa siri kuwa Rais Trump alitumia vibaya msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa sababu binafsi za kisiasa, kumshinikiza rais wa nchi hiyo kwenye mawasiliano kwa njia ya simu, kumchunguza mtoto wa mgombea urais wa chama cha Democrats Bw Joe Biden.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako