• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika zatakiwa kutumia teknolojia mpya kushughulikia ukosefu wa chakula

  (GMT+08:00) 2019-11-01 09:23:49

  Umoja wa Afrika umezihimiza nchi za Afrika zikumbatie teknolojia mpya ili kushughulikia suala la ukosefu wa chakula na utapiamlo barani humo.

  Mwito huo ulitolewa na kamishna wa umoja huo anayeshughulikia uchumi wa vijijini na kilimo Bibi Josefa Sacko, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya 10 ya Usalama wa Chakula na Lishe barani Afrika (ADFNS), ambayo inafanyika nchini ya kauli mbiu ya Kukuza teknolojia mpya za kilimo kwa ajili ya kuboresha lishe barani Afrika.

  Bibi Sacko amesisitiza kuwa maendeleo ya teknolojia za kilimo, chakula na lishe yanaweza kutoa fursa za kubadilisha hali ya ukosefu wa chakula na utapiamlo barani Afrika. Ameongeza kuwa matumizi ya teknolojia za kilimo ni njia ya kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako