• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama la UN larefusha muda wa Tume ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur

  (GMT+08:00) 2019-11-01 09:34:07

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha makubaliano ya kuongeza muda wa Tume ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur kwa mwaka mmoja hadi tarehe31 mwezi Oktoba, mwakani.

  Azimio nambari 2495 lililopitishwa na Baraza hilo limehimiza serikali ya Sudan, vikundi vyenye silaha huko Darfur na wadau wengine wote, kushiriki kikamilifu na kuendeleza mchakato wa amani, na kutaka tume hiyo kuendelea na juhudi za kukuza mchakato wa amani wa Darfur, kuwalinda raia, kufuatilia na kuripoti ukiukaji wa haki za binadamu, kurahisisha msaada wa kibinadamu na kuweka usalama unaofaa kwa wakimbizi kurudi nyumbani mwao au makazi katika nchi ya tatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako