• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yapanga kupeleka polisi wengi zaidi Somalia

  (GMT+08:00) 2019-11-01 09:34:25

  Kiongozi mmoja wa ofisi ya polisi amesema kuwa Uganda imepanga kutuma polisi wengi zaidi kujiunga na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

  Mkurugenzi wa operesheni za kusaidia amani katika kikosi cha polisi cha Uganda Bibi Grace Turyagumanawe amesema kuwa Uganda inafanya maandalizi ya kutuma polisi zaidi ili kuunga mkono usalama wa Somalia.

  Bi. Grace amesema hayo akikutana na naibu mjumbe maalum wa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia suala la Somalia Bw. Simon Mulongo mjini Mogadishu, ameongeza kuwa maandalizi yanaendelea ili kuhakikisha kupeleka polisi wa kundi la pili hivi karibuni.

  Kutokana na Mpango wa Mpito wa Somalia, polisi wa AMISOM wanafanya kazi kuhakikisha Jeshi la Polisi la Somalia kuwa na vifaa vya kutosha, ili liweze kuchukua jukumu kamili la kutekeleza sheria na kulinda utulivu nchini Somalia baada ya ujumbe wa AMISOM kuondoka mwaka 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako