• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la majini la Senegal lakamata tani 1.26 ya mihadarati

  (GMT+08:00) 2019-11-01 09:40:46

  Jeshi la Senegal limekamata tani 1.26 ya Kokeini, kwenye eneo la bahari lililoko kilomita 120 kutoka Dakar, mji mkuu wa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema operesheni hiyo ilitekelezwa kwa pamoja na kikosi maalumu cha jeshi la majini la Senegal na kikosi cha polisi cha Hispania. Meli mbili zilifanyiwa ukaguzi na watu watano walikamatwa. Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa dawa hizo za kulevya zinatoka Latin Amerika na zilipangwa kusafirishwa kwenda Hispania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako